HATUA ZA KUFUATA ILI UTENGENEZE BLOG YAKO MWENYEWE

Website ni dhana na silaha muhimu ya biashara kujitangaza duniani kote,kuelezea huduma au bidhaa ambazo kampuni husika inazo,na njia ya mawasiliano na mahali kampuni ipo,Blog  njia mojawapo ambapo hii ni tofauti na website inampatia mteja nafasi ya ukaribu sana na kampuni husika juu mambo mbalimbali siku hadi siku,mfano huduma mpya,maelezo zaidi ya huduma,kazi mbalimbali za kijamii kampuni inafanya kila siku, nk.Kama unamiliki kampuni,website ni muhimu sana kwa dunia ya sasa,pia ni busara sana kumpatia maelekezo mtengeneza website yako kutengeneza pia blog ya kampuni yenu,kama ni ngumu kutokana gharama kuwa kubwa usijali,unaweza kumiliki blog yako ili uweke ukaribu zaidi na wateja wako kwa kutumia huduma za bure za baadhi  kampuni kubwa sana duniani zinazotoa huduma za blog buree mfano blogspot,wordpress,weebly nk Ukarasa huu nimechagua kuzungumzia hizi blog unaweza tengeneza bure,ambazo ni silaha ya matangazo ya kampuni bila gharama yeyote ile,Karibu.


Zifuatazo ni jinsi ya kutengeneza blog yako kwa kampuni zinazotoa huduma hii bure:

blog 1 

(i)  Tafuta sababu ya kuanzisha blog ,nini dhumuni la kumili hiyo blog,je mambo ya habari,kuelezea matumizi ya bidhaa yako?matangazo,kuelezea kazi za kijamii kampuni yako inafanya,mfuko wa jamii wa kampuni yenu,nk

(ii)    Tengenza  barua pepe yako(e-mail-sign up) ,au kama unayo hii hatua unakuwa haikuhusu.

(iii)  Tafuta kampuni gani unapenda ikupatie huduma ya kumiliki blog yako,zipo kampuni kadhaa,mfano,blogspot,wordpress,webs,weebly,je ungependa blog yako iwena.blogspot.com,wordpress.com,webs.com,mfano,www.tanzaniaachievers.blogspot.com au www.zitto.wordpress.com

(iv)   Baada ya kuchagua kampuni husika ,andika na tafuta(search) neno create free blog kupitia tovuti yawww.google.com, kisha baada ya hapo  bonyeza ,na ingia kampuni ulioichagua hapo hatua ya tatu,kasha  fuata hatua inayofuata.

(v)   Jaza  sehemu ya kuingia kama mwingiaji mpya(sign up),kasha jaza hatua fomu hiyo kwa hatua zote.

(vi)   Baada ya hapo chagua jina la blog unataka iwe,mfano kama umechagua kampuni ya kabla ya .blogspot.com sasa tengeneza jina la blog yako liwe mfano www.issamichuzi.blogspot.com nk kasha angalia upatikanaji wa hilo jina,au kuna mtu analitumia hapo utapewa malekezo na mtandao.

(vii)           Baada ya ujazaji kukamilika sasa blog yako imakamilika na unaweza chagua template utakayo itumia kwa ajili mwonekano wa blog yako,tempelate zipo za bure ndani ya blogspot nk lakini pia unaweza weka yako binafsi,

(viii)         Kama hukuona inapendaza design yako sasa unaweza kuibuni upya kwa kui-design upya tempelate upya,kasha ingia setting kwa minajili kuweka sawa taarifa na mchanganuo mzima wa blog yako,pia unaweza weka kuwa blog yako iwe ya binfsi au umma, nk


(ix)        Sasa unaweza weka taarifa kwa umma kadri unavyoweza


(x)      Fanya mkakati kama ni ya umma ,uitangaze ili ianze kupata watazamaji wengi zaidi kwa kuweka link zako kwa mitandao ya kijamii,chini ya maoni yako kwa tovuti za wengi,pia katika barua pepe zako weka china anuani ya blog yako ili kila anayepata barua pepe yako anaweza ingia kwa blog yako

 By Deogratius Kilawe
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment